Watafiti wa Chuo Kikuu cha Washington cha Marekani wamesanifu simu ya mkononi isiyo na betri, ambayo inaweza kuzalisha umeme kwa mawimbi ya radio au mwanga na inatumia nishati chache sana.
Watafiti wamesema vipuri vyote vya simu hiyo vinaweza kununuliwa sokoni, nguvu ya simu hiyo ni microwatt 3.5. Watafiti wamefanikiwa kuitumia kupiga simu, na kuwasiliana na kituo maalum cha mawasiliano ya simu.
Kwa simu ya mkononi ya kawaida, kubadilisha sauti kuwa ishara ya dijitali kunahitaji nishati nyingi. Nguvu ya vipuri vinavyotumia umeme unaozalishwa kwa mawimbi ya radio au mwanga ni microwatt chache, na haiwezi kukidhi mahitaji ya simu ya mkononi ya kawaida ambayo inahitaji nguvu ya makumi hadi mamia ya miliwati.
Lakini simu hii ya aina mpya inaweza kunasa matetemeko madogo ya mikrofoni, kupokea mawimbi ya radio yanayotoka kwenye kituo cha mawasiliano ya simu, kutia ishara ya mtetemeko kwenye mawimbi na kuyarudisha mawimbi hayo. Mchakato huo unahitaji nishati chache tu.
Majaribio yanaonesha kuwa simu hiyo ikitumia umeme unaozalishwa kwa mawimbi ya radio, inaweza kufanya kazi kwa umbali wa ndani ya mita 9.4 kutoka kituo cha mawasiliano ya simu, na ikitumia umeme unaozalishwa kwa mwanga wa jua, umbali huo utaongezeka kufikia mita 15.2. Hivyo simu hiyo bado haiwezi kutengenezwa kibiashara na inahitaji kuboreshwa zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |