Marekani yawekea raia wa Iran vikwazo vipya
Marekani imewawekea vikwazo vipya raia 18 wa Iran na makundi wanayo yashutumu kusaidia programu ya makombora ya masafa ya marefu ya Iran.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza vikwazo hivyo dhidi ya makundi mawili yanayohusishwa na kikosi maalum cha ulinzi cha Iran, kwa kusema walihusika katika utafiti na utengenezaji wa makombora ya masafa marefu.
Imeendelea kusema kwamba harakati za Iran katika Mashariki ya Kati zinahatarisha uthabiti, usalama na ustawi wa kieneo.
Wakati huo huo, wizara ya fedha ya Marekani imewawekea vikwazo watu watano na taasisi saba kwa kuunga mkono manunuzi ya jeshi la Iran pamoja na raia watatu wengine wa Iran kwa kusema ni sehemu ya kundi la kihalifu lenye makao yake Iran.
Vikwazo hivyo vitazuilia rasilmali za hao Wairan wanaokusudiwa iwapo zinaweza kuwepo Marekani na kuwazuia Wamarekani wasifanye biashara yoyote na watu hao.
Huko Umoja wa Mataifa New York, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Zarif anasema vikwazo hivyo vimekuwa ni tabia mbaya kwa upande wa Marekani, na kwa hivyo Marekani itegemee kuwa Iran italipiza kisasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |