Mawaziri wa nchi za IGAD wakutana kuhimiza amani Sudan Kusini
Mawaziri wa nchi wanachama wa jumuiya ya kimaendeleo ya nchi za Afrika Mashariki IGAD wamekutana mjini Juba, nchini Sudan Kusini kusaidia kufufua mchakato wa amani nchini humo.
Kwenye mkutano huo mawaziri wametaka pande zinazopambana kufanya majadiliano mapana na shirikishi, ili kukomesha mgogoro uliodumu kwa miaka mitatu.
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa nchi za IGAD amewaambia viongozi wa kikanda na mabalozi kuwa, mazungumzo hayo yatasaidia kuleta usimamishwaji vita wa kudumu na kuweka mazingira yanayolazimisha kuwepo kwa majadiliano kati ya makundi yanayopambana.
Mkutano huo wa mawaziri unafuatia mkutano wa viongozi wakuu wa IGAD uliofanya juni 12 mjini Addis Ababa, na kutaka kuwa na mazungumzo ya ngazi ya juu ya pande zote zinazopambana nchini Sudan Kusini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |