• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Binadamu wamezalisha tani bilioni 8.3 za plastiki duniani

    (GMT+08:00) 2017-07-31 18:00:05

    Utafiti mpya uliotolewa kwenye gazeti la Science Advances unasema tangu mwanzoni mwa miaka ya 50 karne iliyopita, binadamu wamezalisha tani bilioni 8.3 za plastiki, ambazo nyingi zimekuwa takataka.

    Kikundi cha watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Georgia, tawi la St. Barbara la Chuo Kikuu cha California, na taasisi ya elimu kuhusu bahari wamefanya utafiti kuhusu uzalishaji, matumizi ya plastiki na takataka za plastiki, wamegundua kuwa mwaka 1950 uzalishaji wa plastiki duniani ulikuwa tani milioni 2, na ifikapo mwaka 2015, uzalishaji huo ulifikia tani milioni 400, ambao ni mkubwa zaidi kuliko vitu vingine isipokuwa saruji na chuma. Miongoni mwa tani bilioni 8.3 za plastiki zilizozalishwa, tani bilioni 6.3 zimekuwa takataka. Na miongoni mwa takataka hizi, asilimia 9 tu zimerudishwa viwandani ili kutumiwa tena, asilimia 12 zimeteketezwa, nyingine asilimia 79 zimezikwa ardhini au kuachiwa katika mazingira yetu. Kwa mujibu wa mwelekeo wa sasa, ifikapo mwaka 2050, kutakuwa na tani bilioni 12 za takataka za plastiki duniani.

    Plastiki nyingi haziwezi kuoza ndani ya muda mfupi, zitakuwepo kwa mamia hata maelfu ya miaka. Mwaka 2010 tani milioni 8 za plastiki ziliingia baharini. Watafiti wamesema binadamu wanatakiwa kufikiri suala la kushughulikia takataka na kudhibiti matumizi ya plastiki kwa makini zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako