Chuo Kikuu cha Oxford kimetoa ripoti kikisema zaidi ya asilimia 60 ya bahari haitunzwi kwa njia mwafaka, na jumuiya ya kimataifa inahitaji kuchukua hatua za dharura ili kuhifadhi viumbe vya baharini.
Ripoti hiyo ilitolewa na watafiti wa chuo hiki kwenye msingi wa utafiti 271 uliotolewa katika miaka mitano iliyopita, imechambua vitisho mbalimbali vinavyokabili viumbe wa baharini, yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, uvuvi kupita kiasi, uchimbaji wa madini baharini, uchafuzi wa kilimo na takataka za plastiki.
Ripoti hii imetoa mfano wa ghuba ya Bengal ikisema viumbe wa ghuba hiyo wako habarini, kwani mabaki ya mbolea yanaendelea kuingia baharini na kuchafua maji, lishe za Nitrates kwenye mbolea zinaufanya mwani kukua kwa wingi baharini, kuvuta Oxygen ya majini na kusababisha samaki na viumbe wengine kukosa Oxygen. Hali hii ikizidi kuwa mbaya, si kama tu viumbe wa ghuba hiyo wataathiriwa, bali pia maeneo mengine ya bahari pia yataathiriwa kutokana na uchafuzi unaoenezwa na mikondo, na mwishowe kuathiri rasilimali za samaki duniani.
Chuo Kikuu cha Oxford kinasema ripoti hii imewasilishwa kwenye mashirika husika ya Umoja wa Mataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |