• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpangaji wa shambulizi la kigaidi la Hispania auawa na polisi

    (GMT+08:00) 2017-08-22 09:36:36

    Polisi wa Hispania wamethibitisha kuwa Younes Abouyaaqoub mwenye umri wa miaka 22 aliyethibitishwa kupanga shambulizi la kigaidi Alhamisi wiki iliyopita lililosababisha vifo vya watu 14 huko Barcelona, alipigwa risasi na polisi jana saa 11 jioni, huko Subirat, mji ulioko kilomita 50 kusini magharibi mwa Barcelona.

    Mwanzoni ilidhaniwa kuwa Younes amekimbia nchi, lakini aligunduliwa jana na kupigwa risasi karibu na eneo la tukio, baada ya kutoroka kwa gari alilopora na kumuua kwa kisu dereva wa gari hilo.

    Habari zinasema washukiwa wengine wanne wa shambulizi hilo wanaoshikiliwa na polisi watafikishwa kwenye Mahakama Kuu ya Hispania leo. Watu hao ni kati ya watu 12 waliohusika na mashambulizi hayo, ambayo pia yalisababisha watu 120 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako