• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watuhumiwa wa ugaidi wafikishwa mahakamani nchini Hispania

    (GMT+08:00) 2017-08-22 19:09:32

    Watuhumiwa wanne walio hai kati ya kundi la watu 12 linaloshukiwa kuhusika na mashambulizi yaliyotokea wiki iliyopita mjini Barcelona na Cambris nchini Hispania wamefikishwa kwenye Mahakama Kuu ya nchi hiyo leo.

    Watuhumiwa wengine watano wa kundi hilo waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini Cambrils, wawili waliuawa katika mlipuko wa gesi mjini Alcanar, na mtuhumiwa mmoja anayeshukiwa kuendesha gari lililowagonga watu mjini Barcelona ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi karibu na mji wa Subirats jana mchana.

    Watu 13 waliuawa na wengine 120 kujeruhiwa alhamis mchana baada ya gari jeupe kupita kwa kasi katika mtaa maarufu wa utalii wa Las Ramblas mjini Barcelona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako