Kutokana na ongezeko la idadi ya watu duniani, mahitaji ya chakula yanaongezeka siku hadi siku. Utafiti mpya unaonesha kuwa ufugaji wa samaki baharini una mustakabali mzuri, na nchi nyingi za pwani zina uwezo wa kutimiza uzalishaji mkubwa zaidi wa samaki. Kikundi cha utafiti kimetoa ripoti kwenye gazeti la Nature Ecology & Evolution la Uingereza kikisema wametafiti data nyingi za mazingira ya baharini na aina 180 za samaki, ili kuchunguza uwezekano wa maendeleo ya ufugaji wa samaki katika sehemu mbalimbali duniani.
Ripoti inasema kuna maeneo mengi ya bahari yanayofaa ufugaji wa samaki duniani ikiwemo Indonesia, Kenya na Fiji. Watu wakitumia vizuri maeneo hayo ya bahari, wataweza kuzalisha tani bilioni 15 za samaki kila mwaka, ambazo ni mara 100 ya mauzo ya samaki duniani ya hivi sasa.
Ripoti hiyo inasema ufugaji wa samaki nchini Marekani pia unstahili kuboreshwa. Inakadiriwa kwamba Marekani ikitumia vizuri asilimia 0.01 ya bahari yake, itaweza kuzalisha samaki wa kutosha kukidhi mahitaji nchini.
Prof. Ben Halpern kutoka Chuo Kikuu cha Imperial cha London ambaye ni mmoja kati ya mwandishi wa ripoti hiyo amesema ufugaji samaki baharini unasaidia kuhakikisha utoaji wa chakula na kusukuma mbele ongezeko la uchumi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |