• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa kuzalisha karatasi kwa vichungi vya sigara nchini Brazil

    (GMT+08:00) 2017-08-31 20:40:45

    Kando ya barabara za miji mingi nchini Brazil kuna masanduku ya rangi ya kijani yenye shimo la duara, ambayo yanatumiwa kuweka vichungi vya sigara. Vichungi hivi vinapelekwa kiwandani na kutumiwa kuzalisha karatasi. Mradi huo wa mzunguko wa takataka ulipendekezwa na Chuo Kikuu cha Brasilia na unaanza kutumiwa katika miji mingi zaidi nchini humo.

    Kiongozi wa mradi huo ambaye pia ni profesa wa Chuo Kikuu cha Brasilia bibi Therese Hoffman amefahamisha kuwa mwanzoni taswira hii ilitolewa na mwanafunzi wa kitivo cha sanaa mwaka 2002, baadaye mwanafunzi huyu na yeye walifanya majaribio mengi, na kugundua kuwa muundo wa vichungi vya sigara unafanana na ubao uliosagwa kwa ajili ya kutengeneza karatasi.

    Baada ya kufanya juhudi kwa mwaka mmoja, Bibi Hoffman alisajili hataza kuhusu teknolojia ya kuzalisha karatasi kwa vichungi vya sigara kwenye shirika la hakimiliki za viwanda la Brazil mwaka 2003, na kusaini makubaliano ya matumizi ya hataza na kampuni moja iliyoko katika jimbo la Sao Paulo mwaka 2014, ili kuiidhinisha kampuni hiyo kushughulikia mzunguko wa vichungi vya sigara na uzalishaji wa karatasi. Hivi sasa masanduku ya kurudisha sigara yamewekwa katika miji mingi ikiwemo Brasilia, Sao Paulo na Campinas.

    Bibi Hoffman amesema kazi muhimu ya kushughulikia vichungi vya sigara kabla ya kuzalisha karatasi ni kuondoa kemikali mbaya na harufu ya sigara. Amesema vichungi vya sigara vinasafishwa na kuweka majini pamoja na kemikali za alkali ikiwemo Sodium Hydroxide, halafu kupashwa moto kwa saa kadhaa. Baadaye vichungi hivi vinabadilika kuwa nyuzi zinazofaa kuzalisha karatasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako