• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mababu wa binadamu huenda walihama kutoka Afrika mapema zaidi

    (GMT+08:00) 2017-09-06 14:26:52

    Kikundi kinachoundwa na watafiti wa Poland na Sweden kimegundua mabaki kadhaa ya nyayo za miguu magharibi mwa kisiwa cha Crete Ugiriki, ambazo huenda ziliachwa na binadamu wa kale walioishi katika miaka milioni 5.7 iliyopita, na kuonesha kwamba mababu wa binadamu huenda walihama kutoka Afrika mapema zaidi.

    Miguu ya binadamu ni tofauti na wanayama wengine wanaoishi kwenye nchi kavu, ambayo ni mirefu, ina vidole vitano vifupi ambavyo vinaelekea mbele, tena haina makucha makali. Miguu ya nyani inafanana zaidi na mikono ya binadamu, ambayo kidole gumba ni kirefu zaidi na kinaelekea upande tofauti na vidole vingine. Hivyo watafiti wanaona kuwa mabaki ya nyayo za miguu waliyoyagundua yanaonekana zaidi kuachwa na binadamu wa kale.

    Kabla ya hapo, wanasayansi wengi walikubali kwamba mababu wa binadamu walizaliwa kwenye mbuga za Afrika, na binadamu wa kale walihama kutoka Afrika katika miaka milioni 2 iliyopita.

    Watafiti wamesema, katika miaka milioni 5.7 iliyopita, jangwa la Sahara lilikuwa bado halipo, na kisiwa cha Crete kilikuwa bado hakijatengwa na bara la Ugiriki, hivyo kuhamia kisiwa hiki kwa binadamu wa kale ni jambo linalowezekana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako