Kila ifikapo majira ya joto, Asia ya Mashariki, bahari ya kusini ya China na Amerika ya Kaskazini hukabiliwa na tufani au vimbunga mara kwa mara. Je, kuna tofauti gani kati ya tufani na kimbunga, na vinapewa majina vipi?
Shirika la hali ya hewa Duniani WMO limeamua kuwa tufani au vimbunga ni dhoruba kali inayoanza katika maeneo ya tropiki yenye upepo wenye kasi ya zaidi ya mita 32.7 kwa sekunde. Lakini kwa kawaida dhoruba zinazotokea kaskazini magharibi mwa bahari ya Pasifiki na bahari ya kusini ya China zinaitwa tufani, na zile zinazotokea kaskazini mashariki mwa bahari ya Pasifiki na bahari ya Atlantiki zinaitwa vimbunga.
Mtabiri wa hali ya hewa kutoka Australia Bw. Clement Wragge aliyefanya kazi mwishoni mwa karne ya 19 hadi mwanzoni mwa karne ya 20 ni mtu wa kwanza kuzipa dhoruba majina, lakini majina aliyochagua ni ya wanasiasa asiyewapenda.
Kuanzia mwaka 1953, kituo cha kimbunga cha Marekani kilianza kuvipa vimbunga majina ya wanawake, na jina la kwanza ni Alice. Kuanzia mwaka 1979, majina ya wanaume yaliongezwa. WMO limetunga orodha 6 za majina ambazo zinatumiwa kila miaka 6.
Nchi zinazoathiriwa na tufani ni nyingi zaidi, zamani nchi tofauti zilitoa majina tofauti kwa tufani. Ili kutatua tatizo la majina, kamati ya tufani ya WMO ilitoa orodha yenye majina 140 ya tufani mwaka 2000.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |