Wanasayansi wa Marekani wamebuni kifaa cha upimaji chenye umbo la kalamu, ambacho kinaweza kutambua ogani za binadamu zinaweza kujitokeza saratani au la ndani ya sekunde 10 na kiwango cha usahihi kimezidi asilimia 96. Njia hiyo inatarajiwa kuwasaidia madaktari kukata uvimbe kwa usahihi kwenye upasuaji.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Texas cha Marekani wamesema, kifaa hicho walichokibuni kinaitwa MasSpecPen, ambacho kasi yake ya upimaji ni mara 150 ya teknolojia iliyopo hivi sasa. Matumizi ya kifaa hicho katika upasuaji yanaweza kuzuia ukataji usio kamilifu kusababisha kutokea tena kwa saratani, na kwa upande mwingine yanaweza kupunguza hasara kwa ogani yenye afya.
Matumizi ya kifaa hicho ni rahisi, unadidimiza kalamu hiyo kwenye ogani kwa sekunde 3, ambayo inaweza kudondosha maji kidogo kukusanya protini, mafuta na vitu vya umetaboli na kupeleka data kwenye kompyuta,
Kutokana na seli za kawaida na seli za saratani zinatoa vitu tofauti vya kikemikali, kompyuta zinaweza kutafiti vitu hivyo na kuonesha matokeo ya upimaji. Watafiti wametumia njia hiyo kupima sampuli 253 za ogani za binadamu, ikiwemo saratani za mapafu, matiti, na uke. Kiwango cha usahihi kinazidi asilimia 96. Watafiti wanapanga kutumia kifaa hicho katika majaribio ya binadamu kuanzia mwaka 2018.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |