Wanasayansi wa Ujerumani wamegundua kuwa njiwa wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja. Uwezo wao unafanana na binadamu, na hata mkubwa zaidi kuliko binadamu。
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Ruhr mjini Bochum Ujerumani wametoa ripoti kwenye gazeti la Current Biology la Marekani ikisema ingawa ndege hana tabaka la nje la ubongo linalofanana na mamalia, lakini kiasi cha neuroni katika milimita moja ya ujazo ya ubongo wa ndege ni mara 6 ya kiasi cha binadamu, hii inamaanisha kuwa umbali kati ya neuroni mbili kwenye ubongo wa ndege ni nusu ya umbali kwenye ubongo wa binadamu. Hivyo wanasayansi wamekadiria kuwa huenda ubongo wa ndege unashughulikia ishara ya neva kwa kasi zaidi kuliko binadamu.
Ili kuthibitisha kadirio hili, watafiti wamewafanya njiwa na binadamu kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja, halafu kuacha kazi ya kwanza na kufanya kazi ya pili mara moja. Katika majaribio hayo, kasi za kugeukia kazi ya pili za njiwa na binadamu zinafanana. Katika majaribio ya pili, watafiti wamewafanya njiwa na binadamu kuacha kazi ya kwanza, kusubiri kwa muda mfupi na kuanza kufanya kazi nyingine, na katika hali hii njiwa anageukia kazi nyingine kwa kasi zaidi kuliko binadamu kwa milisekunde 250.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |