• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Hispania yachukua hatua kukabiliana na kura ya maoni ya jimbo la Catalonia

    (GMT+08:00) 2017-10-03 08:51:46

    Serikali ya Hispania imechukua hatua za dharura kukabiliana na kura ya maoni iliyofanyika Jumapili kuhusu jimbo linalojitawala la Catalonia kujitenga na Hispania.

    Waziri mkuu wa Hispania Bw. Mariano Rajoy ameitisha mkutano wa dharura kujadili suala hilo, pia atakuwa na mazungumzo na viongozi wa chama cha upinzani cha nchi hiyo. Bw. Rajoy amesema, zoezi hilo ni haramu, lakini pia ameeleza kuwa serikali kuu ya Hispania inapenda kufanya mazungumzo na mamlaka ya jimbo hilo.

    Shirika la habari la Ufaransa AFP na vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa, mapambano kati ya polisi na wapiga kura yalitokea baada ya polisi nchini Hispania kufunga baadhi ya vituo vya kupigia kura, na kusababisha watu mia kadhaa kujeruhiwa.

    Kamati ya Umoja wa Ulaya jana imetangaza kuwa kura ya maoni kuhusu kujitenga kwa jimbo la Catalonia si halali kwa mujibu wa katiba ya Hispania, na inazitaka pande zote nchini Hispania zisimamishe makabiliano na kuanzisha mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako