• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfalme wa Hispania alaani kura ya maoni kuhusu jimbo linalojitawala la Catalonia kujitenga na Hispania

    (GMT+08:00) 2017-10-04 19:18:53

    Mfalme Felipe VI wa Hipania amelaani kura ya maoni kuhusu jimbo linalojitawala la Catalonia kujitenga na Hispania, akisema kitendo hicho kimekiuka sheria na kanuni ya kujitawala na kuharibu utulivu na mshikamano wa taifa la Hispania.

    Akihutubia kwa njia ya televisheni kuhusu kura hiyo, Mfalme Felipe VI amesema Hispania inakabiliana na kipindi kigumu katika historia yake ya demokrasia. Amesisitiza kuwa serikali ya jimbo linalojitawala la Catalonia ilikiuka sheria na kanuni ya kujitawala kwa makusudi, na imevunja msingi wa demokrasia ya taifa na masikilizano ya sehemu ya Catalonia, na kufarakanisha jamii ya sehemu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako