Mkuu wa serikali ya jimbo la Catalonia nchini Hispania, Bw. Carles Puidgemont amependekeza kusitisha mchakato wa kutangaza uhuru kwa wiki kadhaa ili kuacha nafasi kwa ajili ya mazungumzo. Bw. Puigdemont amesema hayo jana kwenye bunge la jimbo hilo ambako alishiriki kwenye mkutano wa kutathmini hali ya kisiasa jimboni Catalonia, baada ya kura ya maoni isiyo halali kufanyika Oktoba Mosi. Bw. Puigdemont amesema suala la Catalonia ni suala la Ulaya, na kwamba njia ya pekee ya kupata maendeleo ni kupitia amani na demokrasia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |