China yakabidhi msaada wa dharura kwa Sudan Kusini
Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini wiki hii umekabidhi tani 1,500 za michele na kontena 27 zilizobeba mahema, vyandarua na blanketi kama msaada wa dharura kwa nchi hiyo.
Balozi wa China nchini humo Bw. He Xiangdong amesema awamu ya tatu ya msaada wa mchele uliotolewa na China ni sehemu ya tani 8,800 za michele ambayo China iliahidi kutoa mwezi Aprili ili kuisaidia Sudan Kusini kupambana na uhaba mkubwa wa chakula.
Bw. He ameongeza kuwa, kontena hizo 27 zina mahema 3,700, vyandarua 15,000 na blanketi 30,000 zitaisaidia serikali kuwashughulikia watu waliopoteza makazi na pia kukabiliana na maafa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |