Kikundi cha wanaakiolojia kutoka taasisi ya akiolojia ya mkoa wa Henan na Chuo Kikuu cha Shandong cha China kinafanya uchunguzi wa miezi miwili kuhusu mabaki ya kale ya Kimengich nchini Kenya kuanzia tarehe 1 mwezi Oktoba, ili kutafuta ushahidi wa chanzo cha binadamu wa kisasa.
Mabaki hayo yaliyogunduliwa mwaka jana yako katika eneo la kaunti ya Baringo, yako kwenye eneo lenye milima midogomidogo na miti michache katika bonde la ufa la Afrika Mashariki. Kutokana na kusafishwa na mvua, vyombo vya mawe na mabaki ya mifupa ya wanyama yanaonekana juu ya ardhi.
Mtafiti kutoka taasisi ya akiolojia ya mkoa wa Henan Bw. Li Zhanyang amesema, kwenye sehemu ya juu ya mabaki hayo kuna vyombo vingi vizuri vya mawe na mabaki ya mifupa ya wanyama, katika sehemu ya katikati kuna mashoka, sururu, visu na vipande vya mawe, na kwenye sehemu ya chini zaidi kuna mabaki ya mawe yenye historia ya miaka milioni 2, ambayo huenda ni moja kati ya mabaki ya utamaduni wa binadamu yenye historia ndefu zaidi nchini Kenya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |