Wanasayansi wa China na nchi mbalimbali wameshirikiana kutatua tatizo la muda mrefu la kusukuma vitu kwa kutumia mwanga wa Laser. Utafiti huo umetolewa kwenye gazeti la Science Advances.
Kikundi cha utafiti kinachoundwa na watafiti wa Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia ya elektroniki cha China, Chuo cha uhandisi cha Henan na Chuo kikuu cha Houston cha Marekani kilipofanya majaribio kuhusu chembe ndogondogo za dhahabu zenye kipenyo cha nanomita kadhaa, kimegundua kwa bahati athari ya mwanga kwenye maji. Wanasayansi waliweka chupa ya maji yenye chembe za dhahabu chini ya mwanga wa Laser, baada ya muda, maji hayo yakatiririka kwa kasi yakifuata mtiririko wa mwanga wa Laser. Mwendo kasi wa maji unaweza kufikia sentimita 4 kwa sekunde na kudumu kwa karibu saa moja chini ya mwanga wa Laser wa miliwati 120.
Prof. Wang Zhiming kutoka Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia ya elektroniki amesema chembe za dhahabu zimefanya kazi muhimu kwenye majaribio hayo. Chembe hizi zikiangazwa na mwanga wa Laser wenye mapigo, zinarudia kupanuka na kusinyaa, na kuleta mawimbi ya sauti aina ya ultrasonic, na mawimbi ya sauti yanafanya maji kutiririka kwa kasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |