Wanajimu wamegundua sayari ndogo mbili zinazozungukana zikitoa hewa na vumbi angani kama nyotamkia.
Sayari ndogo ni gimba dogo la angani linalozunguka jua ambazo nyingi zinaundwa na miamba. Nyotamkia ni gimba linaloundwa na mawe, vumbi na barafu, na inapokaribia jua inatoa hewa na vumbi na kuunda mkia.
Kikundi cha utafiti cha kimataifa kinachoongozwa na taasisi ya utafiti wa mfumo wa jua ya Max Planck ya Ujerumani kimechambua data zilizokusanyika kwa kutumia darubini ya Hubble, na kugundua kuwa gimba la 288P lililoko kwenye ukanda wa sayari ndogo kati ya Mars na Jupiter linatoa hewa na vumbi kama nyota mkia.
Uchambuzi zaidi unaonesha kuwa 288P si gimba moja, bali ni sayari ndogo mbili zinazozungukana, ambazo kila moja ina kipenyo cha kilomita 1, na zina umbali wa kilomita 100. Watafiti wamekisia kuwa 288P huenda iligawanyika kuwa sayari ndogo mbili kutokana na athari ya mzunguko katika miaka 5000 iliyopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |