Hivi karibuni watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Cornell na Chuo Kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani wamebuni rasilimali mpya ambayo inaweza kubadilisha rangi na umbo. Watafiti wamesema wamebuni rasilimali hiyo kwa kujifunza kutokana na uwezo wa pweza wa kubadilisha umbo na rangi ya ngozi yake.
Watafiti wametumia rasilimali laini na kuifanya kubadilika umbo lake, lakini ni vigumu sana kutimiza mchakato huo, hivyo wamebuni rasilimali iitwayo CCOARSE, ambayo inaweza kupanua kwa kasi kwa umbo la duara. Kikundi cha watafiti kimewasilisha ombi la hataza.
Ili kuiga uwezo wa pweza, watafiti wameweka wavu ndani ya jeli ya silika, halafu kuamua umbo la rasilimali hii kwa njia maalum ya kuhesabu, na kubadilisha umbo lake kwa mwanga wa Laser.
Ripoti ya utafiti huo itatolewa kwenye gazeti la Sayansi.
Habari zinasema jeshi la nchi kavu la Marekani linafikiri kutenga fedha kuunga mkono mradi huo, kwa sababu teknolojia hii itasaidia roboti na mitambo husika iwe na uwezo wa kujificha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |