• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pterosaur waliwahi kuishi kwa amani na ndege kwa mamilioni ya miaka

    (GMT+08:00) 2017-11-06 09:35:24

    Nadharia ya jadi ya biolojia inasema Pterosaur huenda walitoweka kutokana na ushindani wa ndege. Watafiti wa Australia wamesema nadharia hii huenda imekosea, kwa sababu uhusiano kati ya ndege na Pterosaur ni uhusiano wa kushindana, bali waliishi pamoja kwa amani kwa mamilioni ya miaka.

    Pterosaur waliishi katika miaka milioni 228 hadi milioni 65 iliyopita, na ni watambaazi wanaoweza kuruka. Jina la Pterosaur linatoka lugha ya Kigiriki, ambalo linamaanisha mjusi mwenye mabawa. Pterosaur mkubwa zaidi ana mabawa yenye urefu wa mita 12, na mdogo zaidi ana mabawa ya sentimita 25 tu.

    Mtafiti wa kitivo cha sayansi ya viumbe cha Chuo Kikuu cha Macquarie Bw. Nicholas Chan amesema watafiti wa chuo hiki wamelinganisha urefu wa midomo, mabawa na miguu ya Pterosaur na ndege, na kugundua kuwa sehemu ya katikati ya mabawa ya ndege ni fupi zaidi, miundi ya miguu ni mirefu zaidi na mfupa wa taya mfupi zaidi kuliko Pterosaur. Tofauti hizi zinamaanisha kuwa ndege na Pterosaur wana tabia tofauti kabisa, na kuna uwezekano mdogo wa kushidana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako