• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaspersky yakiri kupakua nyaraka za siri za Marekani

    (GMT+08:00) 2017-11-06 09:36:09

    Kampuni ya usalama wa mtandao ya Kaspersky Lab ya Russia imekiri kuwa iliwahi kupakua kwa bahati mbaya nyaraka za siri za Idara ya usalama ya Marekani NSA wakati ilipofanya kazi za kawaida.

    Hivi karibuni vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa ushahidi umeonesha kuwa kampuni ya Kaspersky Lab iliwahi kuiba nyaraka kutoka kompyuta ya mfanyakazi wa NSA. Kampuni ya Kaspersky Lab imetoa ripoti ikijibu kuwa baada ya kufanya uchunguzi, imegundua kuwa tukio pekee linalohusiana na habari hii lilitokea mwaka 2014. Wakati huo, kampuni hiyo ilikuwa inatafuta kirusi cha "Equation" kwenye mtandao wa Internet. Mchambuzi wa virusi alipochunguza kompyuta ya mteja wa Marekani yenye software ya kukinga virusi ya Kaspersky, aligundua kuwa kompyuta hii inatumia Windows feki, na imeambukizwa na kirusi cha "Equation". Software ya kukinga virusi ilifanya kazi kama kawaida, na kutuma nyaraka zilizoambukiwa kwenye server ya kampuni hiyo ili zichambuliwe.

    Baada ya kuona maneno ya "siri" kwenye nyaraka hizi, mchambuzi wa virusi aliripoti kwa ofisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, na ofisa huyu alimwagiza mchambuzi kufuta kabisa nyaraka hizi, hivyo nyaraka hizi hazipatikani na watu wengine wowote. Baadaye habari zikasema mtu anayemiliki kompyuta hii ni mfanyakazi wa NSA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako