• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njiwa wenye taji watoa kelele ya tahadhari kwa manyoya

    (GMT+08:00) 2017-11-20 16:47:14

    Wanyama wengi wakiwa hatarini, wanalia ili kuwaonya wenzao. Watafiti wa Australia wamegundua kuwa njiwa wenye taji (Crested Pigeon) wanatoa kelele ya tahadhari kwa manyoya maalum badala ya kulia.

    Ndege hao wenye taji jeupe kichwani wanaishi nchini Australia. Watafiti wa Chuo Kikuu cha Australia wamechunguza ndege hao na kugundua kuwa unyoya wa nane kwenye msururu wa manyoya ya mabawa yao ni mwembamba sana, ambao upana wake ni nusu ya unyoya mwingine.

    Watafiti wametafiti zaidi na kugundua kuwa ndege hao wakipeperusha mabawa yao, manyoya membamba yatatoa kelele ya kipekee, na ndege wakipoteza manyoya membamba, hawawezi kutoa kelele ya tahadhari.

    Watafiti wamechambua kuwa ndege hao wamepata manyoya hayo baada ya mabadiliko ya muda mrefu sana, na yanafanya kazi muhimu, ila tu ndege wakipeperusha mabawa kwa kasi ili kuepusha maadui, wataweza kutoa kelele ya tahadhari.

    Ripoti ya utafiti huo imetolewa kwenye gazeti la Current Biology la Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako