• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyangumi wa buluu anaweza kula chakula chenye kalori laki 5

    (GMT+08:00) 2017-11-28 16:59:55

    Nyangumi ni mnyama mkubwa zaidi duniani, ambaye ana uzito sawa na tembo 25. Utafiti unaonesha kuwa nyangumi wa buluu anaweza kugeuka kwa kasi, na kuweza kula chakula chenye kalori laki 5 kwa mkupuko mmoja.

    Kitendo cha nyangumi cha kula kimeonesha upendeleo wake kuhusu upande. Kwa kawaida nyangumi anapenda kugeukia upande wa kulia, lakini video inaonesha kuwa nyangumi anapowinda kamba aina ya krill kwenye sehemu ya juu ya bahari, anageukia upande na kulia, kitendo ambacho ni tofauti na wakati anapowinda samaki katika bahari yenye kina kirefu.

    Mtafiti wa taasisi ya mamalia wa baharini wa Chuo Kikuu cha Oregon Dr. Ari Friedlaender amesema kuna samaki wachache kwenye bahari yenye kina kati ya futi 10 hadi futi 100 kuliko bahari yenye kina kirefu. Nyangumi wanapenda zaidi kugeukia upande wa kushoto ili kuangalia kamba kwa jicho la kulia na kuwawinda kwa ufanisi mkubwa zaidi. Lakini katika bahari yenye kina kirefu iko gizani na kuna kamba wengi, macho ya nyangumi hayasaidii sana, hivyo anapenda kugeukia kulia.

    Dr. Friedlaender amesema huu ni mfano wa kwanza kuhusu wanyama kubadilisha tabia yao ili kuendana na mazingira tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako