Kikundi cha watafiti cha Taasisi ya Kusini Magharibi ya Marekani kimetafiti hali ya dunia katika kipindi cha mwanzo baada ya kuzaliwa kwa njia ya utafiti wa elimumwendo, na kugundua kuwa wakati ule vimondo vingi vyenye ukubwa unaofanana na mwezi viliigonga dunia, na si kama tu viliongeza uzito wa dunia, bali pia vilileta madini yenye thamani kubwa duniani.
Gazeti la ulimwengu la Australia lilifahamisha kuwa vimondo hivi ni vitu vilivyoundwa wakati mfumo wa jua ulipoundwa, ambavyo vile vidogo vilifanana na vumbi, na vile vikubwa vina kipenyo cha kilomita elfu kadhaa.
Watafiti wamegundua kuwa vimondo vikubwa vyenye kipenyo kati ya kilomita 1400 hadi 4400 ambavyo mita moja ya ujazo ya vimondo hivi ina uzito wa tani 4, havikuvunjika juu ya ardhi ya dunia au karibu na dunia, bali viliingia kwenye tabaka la kati na hata kiini cha dunia, na viini vyenye metali vya vimondo hivi vilileta dhahabu, platinamu na fedha duniani.
Utafiti wa zamani ulikadiria kuwa vimondo hivi viliongeza asilimia 0.5 ya uzito wa dunia, lakini utafiti mpya umesema ongezeko hilo huenda ni mara 2 hadi 5 ya lile lililokadiriwa zamani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |