Ni jambo lililozoeleka kukuta mikanda kwenye viti vya magari na ndege, lakini hakuna mikanda kwenye viti vya treni ya kasi. Ukweli ni kwamba hakuna mikanda hiyo kwenye treni zote duniani.
Kuna sababu kadhaa za kutokuwepo kwa mikanda kwenye viti vya treni.
Kwanza, treni za kasi zinakwenda bila kutetemeka hata kidogo. Abiria mmoja aliwahi kufanya majaribio ya kuisimamisha sigara kwenye meza ya treni ambayo iliongeza mwendo kasi hadi kufikia kilomita 300 kwa saa, na sigara hii haikuanguka.
Pili, mikanda kwenye viti vya treni inawadhuru abiria badala ya kuwaokoa. Kamati ya usalama na vigezo vya reli ya Ulaya iliwahi kufanya uchunguzi na kugundua kuwa wakati ajali inapotokea, ni rahisi zaidi kwa abiria wanaofunga mkanda kwenye viti kujeruhiwa kwani hawawezi kutoka.
Na sababu ya tatu ni kwamba abiri hawapendi kufungwa kwenye viti vya treni, wanapenda zaidi kutembea ndani ya mabehewa.
Lakini kwanini tunahitaji kutumia mikanda ya viti kwenye ndege na magari? Ndege inapokumbwa na upepo mkubwa, inatetemeka sana. Kama abiria hawatumii mikanda ya viti, wanaweza kujigonga na paa, viti na sakafu. Na magari yanapogongana au kusimama ghafla, watu watajigonga na usukani, vioo na viti hata kuanguka nje ya magari. Hivyo ni muhimu kufunga mikanda ya viti kwenye ndege na magari.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |