Watafiti wamechunguza maisha ya vijidudu wanaoishi kwenye theluji na barafu ambao wamefunikwa katika ncha za dunia kwa kupima gesi zilizotolewa na vijidudu.
Mwanabiolojia wa Chuo Kikuu cha York cha Uingereza Prof. Kelly Redeker amesema zamani watu hawakuwahi kufikiria athari ya vijidudu kwa mazingira. Lakini ukweli ni kwamba vijidudu vinaweza kupumua na kutoa hewa mbalimbali ikiwemo Carbon Dioxide. Kama kuna hewa hizi kwenye theluji na barafu, inamaanisha kuwa vijidudu vinaweza kuishi na kuzaliana katika mazingira hayo yenye baridi kali.
Watafiti wamezingira eneo la majaribio kwa vitambaa ili kuzuia wanyama pori wasiingie na kuathiri matokeo ya utafiti, halafu wakapima theluji na barafu kwa kutumia taa za mwanga wa UV, na kugundua kuwa kuna kemikali nyingi ya Iodomethane kwenye theluji, na kemikali hii hutolewa na vijijidudu vya baharini.
Hii inamaanisha kuwa vijidudu vinaweza kuishi katika ncha za dunia ambazo zina baridi kali na lishe chache.
Prof Redeker amesema vijidudu vinaweza kuishi kwa mamia na maelfu ya miaka kwenye mazingira yenye baridi kali, katika siku zijazo watatafiti maisha ya vijidudu katika maeneo makubwa zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |