Maneno ya siri bado ni njia muhimu ya kuhifadhi akaunti zetu kwenye mtandao wa Internet. Kila mwaka kampuni ya Splash Data ya Marekani inatangaza orodha ya maneno 25 mabaya zaidi ya siri kwa mujibu wa data za mamilioni ya maneno ya siri zilizofunuliwa. Na mwaka huu neno la siri la "123456" limechukua nafasi ya kwanza tena kwenye orodha hiyo.
Ripoti iliyotolewa na kampuni hiyo inasema maneno matano ya siri yasiyo salama zaidi ya mwaka huu ni "123456", "password", "12345678", "qwerty" na "12345". Ripoti hiyo inasema ingawa neno la siri la "password" haliendani na mpangilio wa keyboard, lakini bado ni baya, na kutumia majina na maneno yoyote yanayopatikana kwenye kamusi si chaguo lenye busara.
Baadhi ya watu wanaweka tarakimu kwenye maneno ili kuyafanya maneno ya siri kuwa salama zaidi, lakini ukweli ni kwamba inategemea mahali pa tarakimu. Kwa mfano, watu wanaandika "passw0rd" badala ya "password", lakini "passw0rd" bado ni kati ya maneno 20 mabaya zaidi ya siri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |