Utafiti mpya uliofanywa pamoja na Australia na Marekani umeonesha kuwa, kufanya mazoezi baada ya kujifunza kunaweza kuimarisha kumbukumbu za mambo uliyojifunza, haswa kwa wanawake.
Watafiti wamawagawanya washiriki 265 wenye umri wa wastani wa miaka 20 kwa vikundi kadhaa kufanya jaribio. Washiriki wa kila kikundi wanatakiwa kukumbuka sura na majina ya watu 15. Baada ya kuziweka akilini, kikundi kimoja kikatakiwa kufanya mazoezi ya kupanda ngazi kwa dakika tano, huku kingine kikifanya mchezo wa meza. Baada ya hapo, washiriki wote walitakiwa kuandika majina wakilinganisha na sura.
Matokeo yameonesha kuwa, kufanya mazoezi baada ya mafunzo kunaweza kuimarisha kumbukumbu za mambo uliyojifunza. Wanawake wanaofanya mazoezi baada ya mafunzo wanafanya vizuri katika kumbukumbu wakilinganishwa na wanawake wasiofanya mazoezi.
Watafiti wamesema, ili kuongeza muda wa watoto darasani, shule nyingi zimepunguza muda wa kufanya mazoezi, lakini mazoezi yanaweza kuwasaidia wanafunzi kuimarisha kumbukumbu. Utafiti huo utazisaidia shule kuweka ratiba za mafunzo na kuinua ufanisi wa kujifunza wa wanafunzi hao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |