Gazeti la Nature la Uingereza limechagua baadhi ya shughuli za kisayansi zinazotazamiwa kutekelezwa katika mwaka 2018.
Binadamu wataendelea kutafiti ulimwengu katika mwaka huu. Mradi wa kupima kiwango cha hydrogen wa Canada utatekelezwa mwaka huu, ambao utawasaidia wanasayansi kutatua masuala kadhaa kuhusu ulimwengu. Mwezi Aprili, wanajimu watachambua mahali na hali ya nyota bilioni 1 za kilimia kupitia data zilizokusanywa na chombo cha uchunguzi wa anga cha Gaia kilichorushwa na Ulaya.
China itarusha chombo cha uchunguzi wa mwezi cha Chang'e-4 ili kuchunguza nyuma ya mwezi. India inapanga kurusha chombo cha Chandrayaan-2 kuchunguza mwezi.
Katika kazi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, nchi mbalimbali zilizosaini makubaliano ya Paris zitaonesha maendeleo mapya katika kutimiza ahadi ya kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani.
Kituo cha utafiti cha nyuklia cha Ulaya kimethibitisha mpango mpya wa kuharakisha chembe, na mpango huo ukifanikiwa, wanasayansi watatengeneza mashine mpya ya mgongano wa chembe.
Kwenye mkutano wa uzito na vipimo wa kimataifa, wajumbe watapitia mswada wa kurekebisha vitengo vya kimataifa, vitengo mbalimbali vikiwemo Kilo, Kelvin, Moore, Ampere vitafafanuliwa tena.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |