• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashine ya uchapishaji wa 3D wa kaure yasanifiwa na taasisi ya teknolojia za viwanda ya Kunshan China

    (GMT+08:00) 2018-01-11 09:29:36

    Taasisi ya teknolojia za viwanda ya Kunshan hivi karibuni imesanifu mashine ya uchapishaji wa 3D wa kaure na malighafi maalum za kaure, na kupata kitambulisho cha vifaa vya matibabu vya kuchapisha meno bandia. Mtu akifungua mdomo na kupigwa picha ya 3D ya meno, mashine hiyo itaweza kuchapisha meno bandia ya Zirconia.

    Kabla ya kuvumbuliwa kwa tenolojia ya uchapishaji wa 3D, watu wakitaka kutengeneza meno bandia, walihitaji kung'ata aina fulani ya udongo ili kurekodi umbo la meno, na viwanda vinahitaji muda mrefu kutengeneza meno bandia. Katika miaka ya hivi karibuni teknolojia ya uchapishaji wa 3D ilianza kutumiwa katika utengenezaji wa meno bandia ya metali, si kama tu imepunguza muda wa utengenezaji, bali pia imebana matumizi ya rasilimali husika. Lakini kuchapisha meno bandia ya kaure bado ni kazi gumu, kwa sababu ni vigumu kuyafanya majimaji ya malighafi ya kaure kuganda ndani ya muda mfupi.

    Taasisi ya teknolojia za viwanda ya Kunshan imetatua tatizo hili kwa kujitegemea, mashine ya uchapishaji wa 3D iliyosanifiwa na taasisi hiyo inaweza kurekebisha nguvu na eneo la mwanga wa Laser wakati wowote, na kuchapisha meno bandia ya Zirconia bila ufa wowote na kwa gharama nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako