Kikundi cha watafiti cha kitivo cha mazingira cha Chuo Kikuu cha Nanjing kikishirikiana na idara mbalimbali za utafiti za China na Marekani, kimetafiti athari ya rasilimali mpya ya Graphene kwa mazingira, na kugundua kuwa viumbe wa juu huenda wakaweza kula rasilimali hiyo kupitia mnyororo wa chakula, na afya huenda ikaathiriwa .
Graphene ni rasilimali nyembamba na ngumu zaidi duniani. Ina unene wa nanomita 0.335 ambao ni moja kwa laki 2 ya kipenyo cha nywele, lakini ugumu wake ni mara 200 ya chuma. Rasilimali hiyo pia ina sifa nzuri katika kupitisha umeme na joto. Lakini matumizi makubwa ya rasilimali hiyo hakika yatasababisha iingie kwenye mazingira ya asili, na kutathimini tisho lake kwa mazingira ni muhimu.
Kikundi cha kitivo cha mazingira cha Chuo Kikuu cha Nanjing kimeanza kutafiti athari ya rasilimali hiyo kwa viumbe mbalimbali wakiwemo samaki aina ya Zebrafish, konokono, minyoo na panya kuanzia mwaka 2011. Utafiti unaonesha kuwa ingawa Graphene nyingi zilizoliwa na samaki baaadaye hutolewa nje ya miili, lakini bado kuna asilimia 1 inaingia kwenye seli za samaki, na moja kwa elfu inaingia kwenye ini.
Graphene inaweza kuathiri viumbe wengi kupitia mnyororo wa chakula. Si kama tu samaki wanaweza kula Graphene moja kwa moja kutoka kwenye mazingira, bali pia wanaweza kuipata kwa kula wadudu waliokula rasilimali hiyo. Hii inamaanisha kuwa Graphene pia inaweza kuingia kwenye mwili wa binadamu baada ya binadamu kula samaki waliochafuliwa na rasilimali hiyo. Na ni rahisi zaidi kwa Graphene kulimbikizwa mwilini kupitia mnyororo wa chakula kuliko kula moja kwa moja kutoka kwenye mazingira.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |