Wanasayansi wamegundua maji na kemikali za kikaboni katika vimondo viwili vyenye historia ndefu kama mfumo wa jua.
Utafiti huo unaongozwa na Dr. Queenie Chan kutoka idara ya sayansi ya sayari na anga ya juu ya Chuo Kikuu Huria cha Uingereza ambaye aliwahi kuwa mtafiti wa Kituo cha anga ya juu cha Johnson cha NASA.
Dr. Chan alisema vimondo viwili vilikusanywa mwaka 1998, ambavyo vimepewa majina ya Monahans na Zag. Vimondo hivi vyote vina chumvi za kibuluu zenye historia zaidi ya miaka bilioni 4.3. Ndani ya chumvi hizi kuna maji na kemikali za kikaboni, ikiwemo asidi ya amino ambayo ni muhimu kwa kuunda protini.
Dr Chan alisema kemikali za kikaboni kutoka kwenye vimondo hivi viwili zinatofautiana, hii inamaanisha kuwa chumvi na vimondo hivi vinatoka sayari tofauti. Alisema chumvi za kibuluu huenda zinatoka sayari bete ya Ceres, kutokana na mlipuko wa volkeno zenye maji au barafu, chumvi hizi ziliingia kwenye anga ya juu na kuanguka kwenye sayari nyingine mbili ndogo ambako ni chanzo cha vimondo hivi viwili.
Dr Chan alisema vimondo hivi vinawapatia watu fusra ya kuelewa mchango wa volkeno zenye maji au barafu, na kuelewa mchakato wa kikemikali wa chanzo cha viumbe.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |