• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baadhi ya ndege wana uwezo wa kuchoma moto ili kujinufaisha

    (GMT+08:00) 2018-01-17 09:39:32

    Watu wengi wanaona kuwa kutumia moto ni uwezo wa kipekee wa binadamu. Lakini wanasayansi wamegundua kuwa baadhi ya ndege wakali wakiwemo mwewe na vipanga wanaoishi nchini Australia wanachoma moto kwa makusudi ili kuwafukuza wanyama wanaojificha kwenye nyasi na vichaka.

    Australia imeshuhudia mara kwa mara ajali za moto zilizosababishwa na ndege ambao walichukua machaka yanayowaka na kuyatupa mahali pengine. Mwanzoni watu walifikiri huenda ndege walifanya hivyo kwa bahati mbaya, lakini watafiti wa Australia wamekusanya ripoti zilizotolewa na wenyeji wanaoishi katika mbuga zenye miti michache za ukanda wa tropiki kaskazini mwa Australia katika miaka 6 iliyopita, na kugundua kuwa ndege huenda wanachoma moto kwa makusudi mara kwa mara.

    Vitendo hivi vya ndege pia vimeripotiwa katika Amerika, Afrika na Asia Kusini, kama ripoti hizi zikithibitishwa, zinamaanisha kuwa ndege wa kanda mbalimbali wamepata uwezo huo wao wenyewe.

    Wataalamu wamesema binadamu walianza kutumia moto katika miaka laki 4 iliyopita, lakini ndege walikuwepo duniani mapema zaidi kuliko binadamu, hivyo huenda walipata uwezo wa kutumia moto mapema kuliko binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako