Kuhamisha kitu kutoka mbali ni jambo linalosimuliwa kwenye hadithi ya sayansi ya kubuniwa, lakini sasa wanasayansi wametimiza jambo hili kwa kutumia mawimbi ya sauti.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Bristol cha Uingereza wametoa tasnifu kwenye gazeti la Physical Review Letters la Marekani wakisema wamefanikiwa kuufanya mpira wa Polystyrene mwenye kipenyo cha sentimita 2 kuelea hewani kwa kizingia cha mawimbi ya sauti yenye marudio ya kilohezi 40 ambacho umbo wake unafanana na kimbunga.
Habari zinasema mawimbi hayo ya sauti si kama tu yanaweza kukifanya kitu kuelea hewani, bali pia yanaweza kuvuta kitu. Kabla ya hapo, watafiti waliwahi kuhamisha kitu kidogo sana kwa mawimbi hayo.
Watafiti wamesema teknolojia hii itaweza kutumiwa katika sekta mbalimbali, kwa mfano kudhibiti vidonge vya dawa au vifaa vidogovidogo vya operesheni vinavyoingia mwilini na kuhamisha vitu vinavyovunjika kwa urahisi. Na baada ya teknolojia hii kuboreshwa siku hadi siku, katika siku zijazo, watu huenda wataweza kuelea hewa kwa mawimbi ya sauti kama hadithi ya sayansi ya kubuniwa inavyoeleza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |