• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watafiti wa Japan watengeneza rasilimali mpya imara kwa magugu maji

    (GMT+08:00) 2018-01-24 16:41:51

    Watafiti wa Japan wametengeneza rasilimali mpya ambayo ni nyepesi zaidi kuliko chuma na ni imara zaidi kwa mara 5 kuliko chuma. Watafiti wamesema rasilimali hiyo ina mustakabali mzuri sana.

    Habari kutoka gazeti la Kyoto Shimbun la Japan zinasema watafiti wa kituo cha teknolojia za viwandani cha mkoa wa Shiga wametengeneza nyuzi za Cellulose zenye kipenyo cha nanomita kadhaa kwa kutumia magugu maji. Kwanza watafiti walitenga kemikali ya Cellulose kutoka ukuta wa seli za magugu, halafu waliifanya iwe nyembamba sana na kutengeneza raslimali nyepesi na imara.

    Kituo hiki kiko karibu na ziwa kubwa la Biwa nchini Japan. Magugu mengi kupita kiasi yamekuwa tatizo la ziwa hilo. Watafiti wanaona kuwa kutengeneza rasilimali mpya kwa kutumia magugu si kama tu kunasaidia kuboresha mazingira ya asili, bali pia kunaleta faida za kiuchumi. Katika siku zijazo wataendelea kutengeneza rasilimali imara ya plastiki kwa nyuzi mseto za Cellulose zenye kipenyo cha nanomita kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako