Wakimbizi 9 wamethibitishwa kufariki na wengine elfu tatu kutengwa kwenye vituo vya matibabu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Uganda.
Mlipuko wa ugonjwa huo ulitokea katika wilaya ya Hoima ambapo wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wanaishi hapa.
Ofisa anayeshughulikia magonjwa wa kuambukiza wa wilaya hiyo Fred Kugonza amesema, ingawa wamechukua hatua za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo, unazidi kuenea kutokana na kuingia kwa wakimbizi wengi kutoka DRC, . Mpaka sasa, hakuna ripoti kuhusu wakazi wa Uganda kuambukizwa na ugonjwa huo.
Bw. Kugonza pia amesema, wizara ya afya ya Uganda inatarajia kutoa taarifa rasmi ya kutokea kwa kipindupindu nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |