Ghala ya mbegu duniani iliyoko kwenye visiwa vya Svalbard kaskazini mwa Norway ilisherehekea miaka 10 tangu ianzishwe tarehe 26 Feburari.
Kwenye sherehe hiyo waziri wa kilimo na chakula wa Norway Bw. Jon Georg Dale amemsema katika miaka 10 iliyopita, akiba za jeni kutoka sehemu mbalimbali duniani zimekuwa zinapeleka sampuli za mbegu kwenye ghala hiyo, na sasa mbegu zinazohifadhiwa huko zimezidi aina milioni 1.
Habari zinasema kabla ya hapo aina laki 9 na elfu 83 za mbegu zimehifadhiwa kwenye ghala hiyo, na baada ya aina elfu 76 za mbegu kupelekwa huko siku hiyo, kwa ujumla kuna aina milioni 1.06 kwenye ghala hiyo.
Ghala ya mbegu duniani ilianza kutumiwa rasmi tarehe 26 Februrari mwaka 2008. Mbegu zinazohifadhiwa huko bado zinamilikiwa kikamilifu na akiba za jeni zilizozipeleka huko.
Ghala hiyo iko chini ya mlima mkubwa karibu na mji wa Longyearbyen. Mbegu zinahifadhiwa huko ili kuzuia mazao ya kilimo yasitoweke kutokana na maafa ya kimaumbile, maradhi, vita na hata "siku ya mwisho ya dunia"
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |