• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ngwini milioni 1.5 wagunduliwa kwenye visiwa vya Danger vya Antaktiki

    (GMT+08:00) 2018-03-07 10:21:26

    Watafiti wamegundua ngwini milioni 1.5 aina ya Adelie kwenye visiwa vya Danger vya Antaktiki. Hili ni kundi kubwa la ngwini ambalo halikujulikana hapo zamani.

    Visiwa hivi 9 viko kwenye bahari iliyoko kaskazini ya peninsula ya Antaktiki. Visiwa hivi vinazingirwa na barafu na ni vigumu kwa meli kupita, hivyo watu wanajua mambo machache kuhusu visiwa hivi.

    Baada ya kuchambua picha zilizopigwa na satilaiti mwaka 2014, wanasayansi waligundua kuwa huenda kuna kundi kubwa la ngwini kwenye visiwa hivi. Mwezi Desemba mwaka 2015 watafiti wa taasisi ya utafiti wa bahari ya Woods Hole na tawi la Stony Brook la Chuo Kikuu cha jimbo la New York walifika kwenye visiwa hivi, na kuanza kuhesabu idadi ya ngwini. Uchambuzi unaonesha kuwa kuna familia laki 7 na elfu 50 za ngwini kwenye visiwa hivi, ambazo ni nyingi zaidi kuliko idadi ya ngwini walioko kwenye sehemu nyingine za peninsula ya Antaktiki.

    Ngwini aina ya Adelie ni ngwini wa kawaida mwenye ukubwa wa kati, wametapakaa katika pwani na visiwa vingi vya Antaktiki. Wana urefu wa sentimita 46 hadi 76 na uzito wa kilo 4 hadi 6. Wanakula kamba na samaki, na wana tabia ya kuishi kwenye makundi makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako