Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Uingereza Vodafone imetangaza kuwa tawi la kampuni hiyo nchini Ujerumani linashirikiana na makampuni kadhaa ili kujenga mtandao wa 4G mwezini mwakani.
Habari kutoka kampuni hiyo zinasema mradi huo utatekelezwa na tawi la kampuni hiyo, kampuni ya mawasiliano ya simu ya Finland Nokia, kampuni ya magari ya Ujerumani Audi na kampuni ya sayansi na teknolojia ya Ujerumani PTScientists.
Kwa mujibu wa mpango, chombo cha uchunguzi wa mwezi cha kampuni ya PTScientists kitapelekwa mwezini kwa roketi ya Falcon 9 katika kituo cha kurushia roketi cha Cape Canaveral huko Florida, Marekani mwakani, na chombo hiki kitachunguza mwezi kwa siku 11.
Wakati huo, magari mawili ya kuchunguza mwezi ya kampuni ya Audi yatakwenda karibu na mahali ambapo gari la uchunguzi wa mwezi la Apollo 17 liliwahi kutua, na kuwasiliana na kifaa cha kutuma na kupokea mawasiliano kwenye chombo cha uchunguzi wa mwezi kwa mtandao wa 4G utakaotolewa na kampuni ya Vodafone, halafu chombo hiki kitatuma data na video ya moja kwa moja duniani. Kifaa hiki cha kutuma na kupokea mawasiliano chenye uzito usiozidi kilo 1 kitatolewa na maabara ya Bell ya kampuni ya Nokia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |