Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Taasisi ya sayansi wa China unaonesha kuwa mimea ilianza kuishi kwenye nchi kavu katika miaka milioni 500 iliyopita, wakati ambao ni mapema zaidi kuliko uliokadiriwa zamani.
Wanasayansi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu lini mimea ya kale ilianza kukua kwenye nchi kavu. Ingawa visukuku vinaweza kutoa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu mabadiliko ya viumbe, lakini ni vigumu kupata visukuku kamili vya kutosha.
Watafiti kutoka Bustani ya mimea ya kitropiki ya Xishuangbanna ya taasisi hiyo na Chuo Kikuu cha Bristol cha Uingereza wametafiti data za transcriptome kwenye seli za aina 103 za mimea na makumi ya visukuku, ili kuhesabu lini mimea ya kale ilianza kuishi kwenye nchi kavu.
Baada ya kuhesabu, watafiti wamesema mimea ya kale ilianza kuishi kwenye nchi kavu katika miaka milioni 500 iliyopita katika kipindi cha Cambrian. Mtafiti Harold Schneider alisema kabla ya hapo, wanasayansi walidhani mimea ilianza kuishi kwenye nchi kavu katika miaka milioni 400 iliyopita, na walisema mimea ya kwanza ya nchi kavu ni kuvumwani, lakini utafiti mpya umekanusha maoni hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |