• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti waonesha kuwa makundi yote ya nyota yanazunguka kwa mzunguko mmoja kila miaka bilioni 1

    (GMT+08:00) 2018-03-23 09:15:26

    Dunia yetu inajizunguka kwa mzunguko mmoja kila siku, inazunguka kando ya jua kwa mzunguko mmoja kila mwaka. Je unajua kundi la nyota na sayari ikiwemo yetu linahitaji miaka mingapi kujizungusha kwa mzunguko mmoja?

    Watafiti wa Kituo cha unajimu wa radio cha Australia ICRAR wametangaza utafiti huo kwenye gazeti la Monthly Notices of the Royal Astronomical Society MNRAS la Uingereza. Utafiti huo unaonesha kuwa mwendo kasi wa kuzunguka kwa kundi la nyota hauhusiani na ukubwa wa kundi la nyota.

    Prof. Gerhardt Meurer wa kituo hiki amesema sehemu ya nje ya kundi la nyota inazunguka kwa mara moja kila miaka bilioni 1 bila kujali ukubwa wa kundi hilo la nyota.

    Profesa huyu amesema makundi tofauti ya nyota yote yanafanya hivyo, na jambo hili litawasaidia wanajimu kuelewa zaidi muundo wa ndani wa makundi ya nyota.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako