Kampuni ya IBM ya Marekani imetangaza kuwa imetengeneza kompyuta ndogo zaidi duniani ambayo ni ndogo zaidi kuliko kidonge kikubwa cha chumvi.
Taasisi ya IBM imefahamisha kuwa gharama ya kutengeneza kompyuta hiyo ni chini ya senti 10, kompyuta hiyo yenye upana wa milimita 1 ina transista milioni 1, inaweza kuchunguza, kuchambua, kutuma na hata kutekeleza data.
Kompyuta hiyo inatumia betri ya nishati ya jua, ina kumbukumbu tuli isiyo na mpangilio maalumu SRAM, na inafanya mawasiliano kupitia LED.
Kampuni hiyo imeonesha kompyuta hiyo kwenye mkutano wa Think 2018 unaofanyika tarehe 19 hadi tarehe 22 Machi huko Las Vegas, Marekani.
Kompyuta hiyo itawekwa kwenye bidhaa ili kurekodi ujumbe mbalimbali kuhusu uzalishaji wa bidhaa hizi. Mkuu wa taasisi ya IBM Bw. Arvind Krishna amesema teknolojia hii itakuwa njia mpya ya kuhakikisha usalama wa vyakula, kuthibitisha bidhaa halisi na feki, na kurekodi viwanda vinavyozalisha bidhaa za anasa.
Kabla ya hapo, kompyuta iliyotengenezwa na chuo kikuu cha Michigan iitwayo "Michigan Micro Mote" yenye upana wa milimita 2 ilikuwa kompyuta ndogo zaidi duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |