Hafla ya kutoa tuzo ya wanasayansi bingwa wa kike duniani ya mwaka 2018 ilifanyika tarehe 22 kwenye makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Paris. Mjumbe wa taasisi ya sayansi ya China ambaye pia ni mtafiti wa taasisi ya wanyama wa kale wenye uti wa mgongo na binadamu wa kale Bibi Zhang Miman na wanasayansi wengine wanne wamepata tuzo hiyo.
UNESCO limesema kazi ya uvumbuzi ya Bibi Zhang imeleta mawazo mapya kuhusu jinsi wanyama wenye uti wa mgongo walivyobadilika kuwa wanyama wa nchi kavu.
Bibi Zhang mwenye umri wa miaka 82 ni mtaalamu maarufu wa samaki wa kale. Mwaka 2016 alipata tuzo ya mafanikio ya maisha ya Romer-Simpson ambayo ni tuzo kubwa zaidi kwa wataalamu wa wanyama wenye uti wa mgongo duniani.
Wanasayansi wengine wanne waliopata tuzo hiyo ni pamoja na mtaalamu wa matibabu ya watoto wa Afrika Kusini Bibi Heather Zar, Mwanabiolojia wa Canada bibi Janet Rossant, mwanabiolojia wa mimea wa Uingereza bibi Caroline Dean and mtaalamu wa ikolojia wa Argentina bibi Amy T. Austin.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |