Raia wa wafukuzwa Australia
Zaidi ya raia wa Ghana 50 waliojaribu kuingia nchini Australia wamekamatwa kwa kujifanya kuwa waandishi wa habari.
Raia hao walishikwa wakati waliposhindwa kujibu maswali kuhusu michezo.
Ingawapo walikuwa na nyalaka halali za kusafiria, walikamatwa na kushikiliwa baada ya kushindwa kujibu maswali rahisi kuhusu michezo.
Naibu Waziri wa Michezo wa Ghana,Pious Enam Hadidze, amesema kuwa wameanza uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Hata hivyo alisema wizara yake haikuwa na uhusiano yoyote na raia hao na haikuwahi kuwasaidia kupata visa hapo awali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |