• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Wakati wa Bo'ao" waanza tena katika majira ya Spring ya mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-04-08 14:22:48

    Katika majira ya Spring ya mwaka 2018, "wakati wa Bo'ao" unaanza tena. Likiwa eneo maalumu kubwa zaidi la kiuchumi na mstari wa mbele wa kutekeleza mageuzi na kufungua mlango nchini China, mkoa wa Hainan unavutia tena macho ya dunia. Miaka mitano iliyopita, rais Xi Jinping wa China alitoa ahadi kwa dunia nzima kwamba China itashikilia kithabiti sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Aprili 10, rais Xi ataeleza mpango wa utekelezaji wa duru mpya ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China kwa dunia.

    China imeamua malengo ya kutimizwa itakapotimia miaka 100 ya kuasisiwa kwa chama na nchi, na kutoa Ndoto ya China ya kutimiza ustawishaji wa taifa la China, hayo yanahitaji kuingizwa nguvu za uhai na msukumo kwa uchumi wa China. Kutokana na juhudi hizi, kasi ya ongezeko la uchumi itaweza kudumishwa kwenye kiwango cha juu cha kuridhisha. Wakati huohuo, China itainua kiwango cha uchumi unaofungua mlango katika maeneo mengi zaidi, nyanja nyingi zaidi na ngazi ya juu zaidi. China inapinga kithabiti aina zote za sera za kujilinda, na kupenda kutatua mvutano wa kibiashara na nchi husika kwa njia ya mazungumzo, ili kuhimiza kujenga utaratibu wa uchumi na biashara wa pande nyingi wenye uwiano, wa kunufaishana na kufuatilia maendeleo.

    China kufungua mlango wake si kwa ajili ya kujenga ua lake binafsi, bali ni kuzinufaisha nchi zote duniani. Katika miaka mitano iliyopita, China na nchi nyingine zimenufaika na matunda ya maendeleo yake kwa pamoja kupitia ushirikiano wa kunufaishana. China imesaini makubaliano ya ushirikiano na nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 40, kuanzisha utaratibu wa kufanya ushirikiano wa kiviwanda na nchi zaidi ya 30, kufanya uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 kwenye nchi zilizopo katika "Ukanda Mmoja, Nija Moja". Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB imezipatia nchi zinazoshiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Nija Moja" mikopo yenye thamani ya dola bilioni 1.7 za kimarekani, na thamani ya uwekezaji kwenye "Mfuko wa Njia ya Hariri" umefikia dola bilioni 4 za kimarekani. Makampuni ya China yamejenga maeneo 56 ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwenye nchi zaidi ya 20, na kulipa kodi ya dola bilioni 1.1 za kimarekani na kutoa nafasi laki 1.8 za ajira katika nchi hizo.

    Kuhusu jinsi ya kukabiliana na maendeleo ya kasi ya mafungamano ya kiuchumi duniani na ushindani mkali wa nguvu za jumla za kitaifa, Xi Jinping alisema kwa uwazi alipohojiwa na Televisheni ya Russia kuwa mageuzi na kufungua mlango vinahitajika kama China ikitaka kutumia vizuri fursa na kupata maendeleo zaidi. Nchi moja yenye watu bilioni 1.3 inataka kutimiza mambo ya kisasa, hapa hakuna mfano wa kuigwa katika historia ya binadamu. China inatakiwa kufuata njia yake ya kipekee katika kutafuta maendeleo, "kuvuka mto kwa kugusa mawe", ili kuimarisha mageuzi na kufungua mlango zaidi, na kutafuta njia ya kusonga mbele. Yamefika majira mengine mapya ya Spring, ikiwa katika shughuli ya kwanza ya kidiplomasia inayoandaliwa na China mwaka huu, dunia nzima inapenda kusikiliza sauti ya China katika zama mpya huko Bo'ao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako