Utafiti mpya unaonesha kuwa uwezo wa ndege wa kutambua ugasumaku wa dunia huenda unahusiana na protini kwenye macho.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Lund cha Sweden wametafiti protini mbalimbali kwenye macho ya ndege aina ya zebra finch, na kugundua kuwa tofauti na protini nyingine, kiasi cha protini aina ya Cry4 hakibadilikibadiliki katika nyakati tofauti za siku moja zenye kiwango tofauti za mwanga wa jua.
Protini aina ya Cry4 inadhibiti mzunguko wa kulala na kuamka (circadian rhythm), lakini baadhi ya utafiti unaonesha kuwa protini hiyo pia inaweza kuhisi ugasumaku.
Watafiti wamesema protini hiyo ambayo kiasi chake hakibadiliki sana ni kitu kizuri cha kuhisi ugasumaku katika wakati wowote.
Watafiti pia wamegundua kuwa, si kama tu ndege wanaohamahama wanahitaji kuthibitisha upande kwa mujibu wa ugasumaku, ndege wanaokaa katika sehemu moja pia wanafanya hivyo.
Mtafiti Atticus Pinzon-Rodriguez amesema huenda wanyama wote wana kitu cha kuhisi ugasumaku miilini mwao, wanahitaji kufanya utafiti zaidi ili kujua jinsi wanyama wanavyohisi ugasumaku na kuthibitisha upande.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |