• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wasumbua mpangilio wa jeni na DNA zisizofanya kazi wa nyangumi wa jamii ya Baleen

    (GMT+08:00) 2018-04-13 08:42:19

    Watafiti wa Ujerumani na Sweden wamesumbua mpangilio kamili wa jeni na DNA zisizofanya kazi (genome) wa nyangumi wa familia ya Baleen.

    Nyangumi wa jamii ya Baleen ni pamoja na nyangumi wa kibuluu, nyangumi kibyongo, nyangumi wa kijivu, na nyangumi pezimgongo-refu. Na nyangumi wa kibuluu ni mkubwa sana, ambao urefu wake unaweza kufikia mita 30 na uzito wake unaweza kufikia tani 175.

    Mtafiti Fritjof Lammers kutoka taasisi ya utafiti kuhusu kuwepo kwa aina nyingi za viumbe na hali ya hewa ya Senckenberg amesema kwa kawaida viumbe wa aina moja hubadilika kuwa viumbe wa aina mbili baada ya kugawanyika na kutoweza kuzaliana kutokana na vizuizi vya kijiografia au jeni, lakini sababu hizi haziwezekani kwa nyangumi wa Baleen, kwani nyangumi wanahamahama baharini. Utafiti wa mpangilio wa jeni na DNA zisizofanya kazi unaonesha kuwa nyangumi wa Baleen wa aina mbalimbali wa jamii ya baleen waliwahi kuzaliana, hivyo uhusiano kati yao una utatanishi mkubwa zaidi kuliko watu walivyofikiri. Kwa mfano, nyangumi kibyongo ana mapezi marefu zaidi kuliko nyangumi wengine wa jamii ya Baleen, utafiti unaonesha kuwa ni kweli nyangumi huyu ana uhusiano wa mbali zaidi na nyangumi wengine, na nyangumi wa kijivu pia ana sura tofauti, lakini utafiti unaonesha kuwa huyu ni nyangumi halisi wa jamii ya Baleen.

    Watafiti wamesema teknolojia ya kupima mpangilio wa jeni na DNA zisizofanya kazi ina mustakabali mzuri, inaweza kufichua mchakato wa mabadiliko ya viumbe mbalimbali kwenye historia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako