Tume maalum ya bunge la Uingereza imetoa ripoti ikisema maadili yanatakiwa kupewa kipaumbele kwenye maendeleo na matumizi ya teknolojai ya akili bandia, ili kuhakikisha teknolojia hii inawanufaisha zaidi binadamu.
Ripoti hiyo iliyoandikwa na kutangazwa na kamati maalum ya akili bandia ya baraza la juu la bunge la Uingereza imefuatilia mustakabali wa teknolojia ya akili bandia na mabadiliko na hatari ambazo zinaweza kutokana na teknolojia hii.
Ripoti hiyo inasema kanuni za akili bandia zinazofaa sekta mbalimbali zinatakiwa kutungwa, ambazo zitahusu pande tano, yaani teknolojia hii inatakiwa kuhudumia maslahi ya pamoja ya akili bandia; inatakiwa kufuata kanuni ya kueleweka na yenye usawa; haipaswi kuingilia faragha za watu, familia na mitaa; raia wote wana haki ya kupata elimu husika ili kuendana na maendeleo ya teknolojia hii; teknolojia hii kamwe haitakiwi kupata uwezo wa kuwadhuru, kuwaangamiza na kuwadanganya binadamu.
Hivi karibuni kampuni ya Facebook ilikumbwa na kashfa ya kufichuliwa kwa data za watumiaji. Ripoti hiyo inasema watu wanatakiwa kupewa haki nyingi zaidi kudhibiti data zao, na njia ya kukusanya data inatakiwa kurekebisha, ili kulinda vizuri zaidi faragha za watu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |